" /> Ugonjwa wa Saratani Katika Kenya – Svast

Habari kuhusu viwango vya saratani hivi sasa nchini Kenya

Ugonjwa wa saratani ni shida kuu ulimwenguni inayosababisha maafa kuliko hata malaria, ukimwi na kifua kikuu zikijuhishwa kwa pamoja. Kulingana na repoti ya shirika la Kenya Network of Cancer, asilimia 70 ya ulimwengu wa saratani inapatikana kwenye nchi ambazo zina mapato ya chini na ya kati kama Kenya.    

Kati ya sababu ya vifo nchini Kenya, saratani iko kwenye nafasi ya tatu na asilimia saba ya vifo vinavyo ripotiwa kila mwaka. Hii ni kulingana na ripoti ya (IAEA, 2010), baada ya magonjwa ya kuambukiza na magonjwa ya moyo katika nafasi ya kwanza na pili mutawalia. Hata hivyo, ni vigumu kupata idadi sahihi ya kitaifa ya wagonjwa wa saratani kwa sababu idadi nyingi hutoka kwenye mipangilio ya miji kama vile Nairobi.    

Makadirio ya kesi mpya za saratani 39000 na vifo 27000 kila mwaka vya ripotiwa. Hii ni kulingana na repoti ya IAEA ya mwaka wa 2010. Takwimu zinaonyesha kuwa karibu wakenya 50 huaga dunia kutokana na aina tofauti za saratani kila siku. Kwa hiyo,takwimu za wizara ya afya zinaonyesha kwamba angalau wakenya 40,000 wanapatikana na magonjwa ya saratani nchini kote.  

Kulingana na ripoti ya takwimu za saratani ya mwaka wa 2018, kuna takiribani visa 1,998 vya saratani zilizoripotiwa mwaka wa 2017. Hii inawakilisha asilimia 5 ya matukio ya mwaka nchini Kenya. Saratani zinayoongoza kwa wanawake kulingana na ripoti ni saratani ya umio (15.1/100,000), saratani ya matiti (31.6/100,000), na  saratani ya mlongo wa uzazi (40.1/100,000). Wakati huohuo, saratani inayoongoza kwa wanaume ni saratani ya kibofu (31.6/100,000), saratani ya umio (20.5/100,00), na Kaposi sarcoma (16/100,000).      

Saratani husababisha changamoto ya kipekee kwa miundombinu ya afya nchini Kenya. Hii ni kwa sababu inaathiri idadi ya vijana zaidi kuliko mahali popote ulimwenguni. Zaidi ya hayo kuna vifaa vichache vya uchunguzi wa  saratani, kuku kukiwa na idadi ya vituo vinne tu huko Nairobi. Hizi ni pamoja na hospitali ya Aga Khan, hospitali ya Nairobi, hospitali ya MP Shah, na hospitali kuu  ya  Kenyata. Pia, kuna uwezo mdogo wa wataalum wa matibabu ya  saratani katika sekta ya uma nchini Kenya, kukiwa na takribani:-

·       wanafikia wawili wa matibabu

·       Wauuguzi watatu wa oncologi

·       Wataalamu watano wa tiba ya teknolojia ya mionzi

·       Oncologisti wanne wa watoto

·       Oncologisti sita wa matibabu

·       Oncologisti wanne wa mionzi           

Wagonjwa wa saratani walio chini ya bima nchini Kenya

Bima ya hospitali ya kitaifa kwa wagonjwa wa saratani ilizinduliwa mnamo mwaka wa 2015. Hii ni kulingana na afisa mkuu mtendaji wa bima ya hospitali ya kitaifa, bwana Geoffrey Mwangi. Chini ya mpango huu, wagonjwa wana haki ya kliniki kila mwezi kuangaliwa, uchunguzi wa MRI na CT scan, radiotherapy na chemotherapy. Kulingana na ripoti ya shirika la afya duniani ya mwaka wa 2018, mfuko wa bima ya hospitali ya kitaifa hufanya matibabu ya saratani karibu kuwa ya bure kwa asilimia 18 ya wakenya walio chini ya mpango huo.   

Katika mwaka wa 2015, bima ya kitaifa ya hospitali ilizindua kufidiwa kwa hadi dola 50,000 za marekani kwa wagonjwa wa saratani waliohitaji matibabu nnje ya nchi. Hata hivyo, mpangilio huu ulirekebishwa mwaka wa 2016 ili kufidia pia wagonjwa saratani waliohitaji kutibiwa nchini Kenya. Kwa kweli ripoti rasmi inaonyesha bima ya kitaifa ya hospitali ilitumia takribani bilioni dola 0.0136 za marekani kwenye mwaka wa kifedha wa 2017/2018 kama malipo kwa matibabu ya saratani (wakijumuisha ndani na wale wa kutiwa nje ya nchi).   

Kwa sasa mfuko wa bima ya kitaifa ya hospitali uhusisha hadi vipimo 10 vya chemotherapy,sindano au dawa ya kupambana na kansa ya mdomo,wagonjwa wa ndani na nje ya huduma ya oncology, hadi vipindi viwili vya brachytherapy kwa saratani iliozidi kipimo, pia vipindi 20 vya radiotherapy kila mwaka.  

Wagonjwa wa kansa ambao wanapaswa kulipa wenyewe

Matibabu ya kansa ni ghali na mara nyingi  hupita hadi  milioni za shilingi za Kenya. Kwa hivyo wagonjwa wengi lazima wategemee dhana ya Kenya ya ‘harambee’(msaada wa jamii binafsi au umati); dhana ya kupata fedha kwa wasiojiweza.


Sara hana kizuizi cha NHIF kwa hiyo imetangaza hii flier kwa fedha za watu
Sarah hana bila ya afya kwa hivyo alitengeneza picha hii ili kupata fedha kupitia mfumo wa harambee.
Rejeleo: tuvuti ya www.tuko.co.ke

Fauzia Aboud (kwenye picha chini) kutoka Mombasa alianzisha matibatu yake ya HER2  kwa faragha  lakini alilazimishwa kuacha kwa sababu fedha kutoka bila ya afya iliisha. Jamaa na marafiki walifanya mchango kwenye harambee ili aweze kuendelea na matibabu yake. Lakini hazikutosha ili aendeleze matibabu yake. Dada yake alimtambulisha kwa mpango wa Innovative public-private partnership ilioko katika hospitali kuu ya Kenyata mjini Nairobi. Kupitia mpango huu Fausa aliweza kukamilisha viwango vilikuwa vimezalia na akabainika kuwa huru kutokana na saratani ya matiti.     


Baada ya kupatikana na saratani ya matiti Fauzia (katikati) alikaribia familia kwa msaada.
Rejeleo: tuvuti ya www.roche.com

Mfadhiliwa mwingine kwenye mpango wa Innovative public-private partnership ilioko katika hospitali kuu ya Kenyata ni Rosa (kwenye picha chini). yeye alitambulishwa kwenye mpango huu na oncologist wake kufanya tiba ya homoni ya HER2-chanya. Hii ni baada ya hiyo zoezi kuwa ghali kwake kugharimia. Hata hivyo alikuwa mwenye furaha baada ya kugundua kuwa angeongoja tu wiki moja kuanzisha matibabu yake katika hospitali kuu ya Kenyata.   


Rejeleo: tuvuti ya www.roche.com

Mpango huu kwenye hospitali kuu ya kenyata ilikusuhudia kuwawezesha wahadhiriwa wa janga la saratani kupata matibabu na tathmini wa saratani kwa wakati unaofaa na kwa urahisi. Mbali na hatua hiyo, serikali ya Kenya  na tahasisi ya Roche Kenya wako na mkataba wa maelewano kuwasaidia kupunguza gharama ya juu ya HER-2 chanya kwa matibabu katika mashika ya kitafaifa. Kulingana na mkugenzi mkuu wa mpango huu, dhamira ya mpango huu ilikuwa kujenga miundo msingi imara ya kuweza kudhibiti matibabu ya saratani nchini Kenya. Ni katika mpango ambapo Bi Fuasa Aboud na Rosa walisaiska kupata matibabu ya HER-2 chanya licha ya gharama ya juu ya matibabu.


Wafadhiliwa wa mpango mahususi wa hospitali kuu ya kenyata kwa matibabu ya matibabu ya HER-2 chanya
Rejeleo: tuvuti ya www.roche.com

Kulingana na ripoti rasmi za sherikali, Kenya hupoteza takriba pesa bilioni kumi na moja kila mwaka ili kuwazesha wakenya husafirin mataifa ya kigeni ili kupata matibabu spesheli dhiti ya ugonjwa ya seretani. Takwimu katika wizara ya afya inaonyesha kuwa angalau wagonjwa 116 walisafiri India kati ya mwezi wa Januari na Machi mwaka wa 2017 kutibiwa ugonjwa wa saratani. Aidha, ripoti zinaonyesha kuwa taifa la India limedhaminiwa sana walimwenguni na pia huduma zake ni za bei nafuu ikilinganishwa na mataifa mengine kama Marekani and Uingereza.          

Geofry Moenga ni miongoni mwa wagonjwa waliotafuta matibabu katika taifa la India. Kwanga alipimwa katika hospitali moja Nairobi na alipatina na vidonda vya tumbo (yaani ulcers kwa kimombo), mwishowe akapatikana na ungoniwa wa herenia. Katika mwaka wa 2012 alifanyiwa upasuaji kwenye hospitali moja nchini Kenya na alipatikana na uvimbe katika maini na kasha ikatolewa.

Alifikiria kutafuta matibabu spesheli nchini India licha ya changa moto ya kifedha. Alikuwa ametumia pesa zote na hakuna kilichosalia kushugulikia matibabu yake kule India. Alizungumza na familia na marafiki zake wakakubali kupanga harambee ili kuchangisha fedha hizo. Aliulizia kwenye chama cha Agile Global Health ili kutathmini kituo mwafaka cha afya na gharama iliyohitajika kule India. Harambee iliofanywa kule Nairobi ilifanikiwa kuchanga asilimia ishirini na tano (25%) ya matibabu kasha akachukua mkopo kwenye chama cha uegezaji cha Kentours iliyoshughulikia gharama iliosalia. Alipokuwa India, matibabu yalifanywa na akadhibitishiwa alikuwa amepona kutokana na saratani ya maini.   

Jane Muthoni, mwalimu, vilevile ni mmoja wapo wa waadhiriwa wa ugonjwa wa saratani waliytafuta matibabu nchini India. Alipatikana na saratani ya tezi mnamo mwaka wa 2002. Alifanyiwa upasuaji katika hospitali nchini Kenya lakini madaktari hawakuweza kutoa uvimbe uliyohuwa umekwama katika koromeo yake. Kwa hiyo, seli za saratani zilianza huenea and kuathiri mabomba yake ya chakula sanduku sauti, na kuenea hadi kwenye napafu yake ya kifua.

Ilisemekana kuwa maisha ya Jane yalikuwa hatarini. Wakati huo, hakukuwepo na bima ya afya kwa wagonjwa wa saratani. Kwa hivyo ilimbidi ategemee marafiki, familia ili kufanya harambee kupata fedha za kugharamia mwendo wake wa kwenda nchini india kwa matibabu.  Aliandamana na bwanake hadi India kwa matibabu hayo spesheli. Madaktari walichukulia hali yake kama changamoto na kutumia mbinu mbalimbali kwa kushirikisha wapasauji wa shingo and kichwa, wapasuaji wa kifua, na wapasuaji wa utumbo ili kufanikisha upasuahi huo.    

Upasuaji ulichukua takribani saa kumi na tano. Madaktari walifaulu kutoa uvimbe na kumuosha kifua, koromeo na glota. Glota ilikarabatia kwa kutumia tubu kutoka kwa tumbo. Alidhibitishiwa kuwa mzima kutokana na saratani tezi.